Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wa Mkonge wakaribishwa kujifunza kilimo cha faida 77

Mkonge Cas Wakulima wa Mkonge wakaribishwa kujifunza kilimo cha faida 77

Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Mkonge Tanzania imehamasisha wananchi kulima zao la Mkonge kwa wingi kwasababu soko lake ni kubwa na la uhakika.

Aidha, kiwango cha uzalishaji wa zao hilo bado ni kidogo kwasababu wakulima wengi hawazingatii kanuni za kilimo cha zao ho.

Ofisa Masoko, Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) David Maghali, ameyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao lililopo katika Maonesho 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.

Maghali amewakaribisha wakulima wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta hiyo kuingia mwenye zao hilo linalovunwa miaka mitatu baada ya kupandwa.

"Mkonge una fursa nyingi ukiachana na kilimo unaweza kuwekeza kwenye mashine za uchakataji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kilimo. Kwa yoyote anayetaka kuwekeza kwenye kilimo hiki tunamkaribisha kwenye banda letu hala sabasaba tuwekeze kumwelekeza aweze kunufaika na fursa zilizopo," amesema Maghali.

Kuhusu changamoto amesema wakulima wengi hawazingatii kanuni za kilimo ikiwamo kutumia eneo kubwa kwa kilimo na kupata mazao machache.

"Kilimo bora ni kuandaa shamba kwa kuondoa visiki na kupitisha trekta pamoja na kupalilia mara tatu hadi nne kwa mwaka ili majani au miti isizonge mmea," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live