Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Wananchi watoa maoni tofauti kauli ya Lukuvi kuhusu ulipaji kodi ya nyumba

Video Archive
Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wananchi wametoa maombi tofauti kuhusu kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania, William Lukuvi aliyesema kuwa mpangaji hapaswi kulazimishwa kulipa kodi ya nyumba kwa miezi sita au 12.

Lukuvi alitoa kauli hiyo juzi Jumanne Novemba 26, 2019 alipokutana na menejimenti ya Shirika la Nyumba Tanzania (NHC).

“Upangishaji ni mkataba kati ya mwenye nyumba na mpangaji, nchi hii tusingependa mpangaji alazimishwe kutozwa kodi ya miezi 12.”

“NHC inawatoza mwezi mmoja na wapo wenye hiari  kulipa mwaka mmoja au miwili. Mwingine ana hiari kulipa mwezi mmoja lazima aruhusiwe kupanga katika nyumba zote binafsi,” amesema Lukuvi.

Kauli ya waziri huyo imeibua maoni tofauti katika mitandao ya kijamii ambapo, Thomas-mika-Simon amesema, “kama Serikali mna hiyo huruma jengeni nyumba ndio muwapangishe mtakavyo nyie mbona biashara nyingine hampangi  ziuzwe kama viwanja, mabati, suruali nakadhalika.”

“Hapo mnachukua kodi yenu vifaa vya ujenzi vipo juu ila kodi mwenye nyumba apangiwe.”

Ibrahimjamesir amesema, “mmoja kati ya viongozi waliobakia ninayemkubali  ni Lukuvi, Lipumba (Profesa Ibrahim- mwenyekiti wa CUF) alisema CCM hata ukipeleka kitu gani ni kama kumtia samaki mzima kwenye kapu la samaki waliooza napenda kumwambia sio, Lukuvi namkubali sana hongera Lukuvi.”

Naye Ndemwita ameandika, “siasa nyepesi kabisa hiyo sheria itakuwepo kwenye makaratasi tu kwani wapangaji wanatofautiana uwezo mimi  kama mwenye nyumba nitachukua mwenye pesa za kunisaidia na sio kwa mujibu wa sheria zenu.”

Kwa upande wake Kentlambo amesema, “kuna malalamiko kutoka kwa wapangaji juu ya huu utaratibu wa kulipa miezi 6 ? Kama hayapo basi sheria inakuwaje tena.”

Samalmokiwa amesema, “naomba Waziri utoe bei elekezi maana hawa jamaa wanatusumbua sana kwa kweli tafadhali mwambie Rais (John Magufuli) atoe bei elekezi wanyonge tunanyongwa sana.”

Chanzo: mwananchi.co.tz