Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO : Tanzania yafafanua masharti ya kusafirisha dola

Video Archive
Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga amesema si kweli kwamba masharti ya Tanzania ya kusafirisha dola ni magumu bali ni masharti magumu katika kila nchi ambayo unapeleka fedha hizo.

Profesa Luoga ameyasema hayo leo Jumatatu Aprili Mosi, 2019 wakati yeye pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango walipokuwa wakitoa ufafanuzi kuhusu ukaguzi wa maduka ya kubadilishia fedha za kigeni.

Amesema masharti ya kusafirisha dola yameendelea kubaki katika Sheria tangu mwaka 1992 na masharti hayo si kwa Tanzania pekee bali na kwa nchi nyingine.

“Kwa mfano unaposafirisha dola kutoka Tanzania inategemea unazipeleka wapi. Marekani huruhusiwi kuingiza zaidi ya dola 10,000 na ukipeleka Uingereza nacho kuna kiwango hicho hicho, ambacho huwezi kuruhusiwa kwenda nacho,” amesema.

Amesema pesa ambayo unaruhusiwa kutoka nayo nchini ni ile ambayo unaruhusiwa kuingia nayo katika nchi nyingine.

“Si kweli kwamba masharti ya Tanzania ni magumu bali masharti ya kila nchi unayokwenda ni magumu katika kubeba dola zako kupeleka kwako. Ukikutwa na dola 400, 000 kwa mfano swali ni kwamba utaenda kuingiza vipi kwenye nchi unayokwenda? Ambayo haitakuruhusu kuingiza zaidi ya dola 10,000,” amesema.

Amesema ina maana mtu huyo kuna mahali ataingia na kufanya shughuli ambayo ni haramu za kuhakikisha kuwa unaingiza fedha hizo katika nchi nyingine.

Alipoulizwa kuhusu ukaguzi katika mikoa mingine mbali na Arusha na Dar es Salaam, Profesa Luoga amesema walianza kazi hiyo Mkoa wa Kilimanjaro lakini hawakumalizia na bado wanaendelea na ukaguzi huo.

Amesema mikoa mingine wameshafanya ukaguzi huo na wamiliki walishapewa notice wale ambao hawakidhi masharti yote watafungiwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz