Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Serikali ya Tanzania yazungumzia uboreshaji mazingira ya biashara

Video Archive
Mon, 2 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Innocent Bashungwa amesema Serikali itachukua hatua muhimu kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini kwa lengo la kukuza uwekezaji.

Amesema hilo litaifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo mwaka 2025.

Bashungwa amebainisha hayo leo Jumamosi Agosti 31,  2019 katika mkutano wa Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI).

“Serikali tunafanya juhudi kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara hapa nchini kuwa ya kuvutia ili kufanikisha safari yetu ya uchumi wa viwanda, ndio maana tunakusudia kupitia sheria, kanuni na sera zetu mbalimbali ambazo tunaona sasa hazina nafasi,” amesema Bashungwa.

Amesema Serikali inataka Tanzania kuwa kituo cha uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa kwa ajili ya jumuiya za kibiashara ambazo ni nchi mwanachama, kwamba  wawekezaji wakiwemo wenye viwanda wanapaswa kutumia fursa hiyo.

 

Pia Soma

Advertisement   ?
“Tunaboresha miundombinu ya usafirishaji, nishati na huduma katika mamlaka mbalimbali za usimamizi. Tunataka mifumo ndio imhudumie mtu lakini sio mtu anapata huduma kwa kwa sababu anafahamiana na mtu fulani serikalini,” amesema.

Amesema wawekezaji waliopo nchini wanatakiwa kuwa mabalozi wa Tanzania katika kuwavutia wawekezaji wengi na kuna fursa ya kufanya ubia na Serikali itawaunga mkono.

Awali, makamu wa Rais wa CTI,  Paul Makanza amesema changamoto ya maendeleo ya viwanda ni pamoja na bidhaa zisizo na ubora, kuchelewa kwa vibali vya kazi vya wataalamu kutoka nje ya nchi, upatikanaji wa mikopo na kuchelewa kwa marejesho ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

“Nchi nyingi zilizoendelea zilifanikishwa na viwanda nasi hatuna budi wala hatuwezi kuepuka hilo, mchango wa sekta ya viwanda katika nchi ni mkubwa. Mwaka 2018 ukuaji wa sekta ya viwanda ulikuwa asilimia 8.3 na ulitoa ajira kwa watu zaidi ya Sh300, 000,” amesema Makanza.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz