Dar es Salaam. Wakala wa Ndege za Serikali ya Tanzania (TGFA) na kampuni ya kutengeneza ndege ya Canada-'De Havilland' wamesaini mkataba wa ununuzi wa ndege moja aina ya Bombardier Q400.
Mkataba huo umesainiwa leo Jumamosi Oktoba 19, 2019 lengo likiwa ni kuimarisha na kuboresha utoaji huduma za usafiri wa anga nchini kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
Mtendaji mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali, Dk Benjamin Ndimila amesema ndege hiyo itakua na uwezo wa kutua hata kwenye viwanja vya vumbi.
"Ndege hii mpya inatarajiwa kufika nchini kati ya Juni au Julai 2019, " amesema Dk Benjamin licha ya kutoeleza imenunuliwa kiasi gani.
Tangu 2016 Serikali imekuwa ikinunua ndege na hivi karibuni
inatarajia kuongeza ndege nyingine tatu.
Pia Soma
- VIDEO: Serikali ya Tanzania yazungumzia wizi wa kompyuta ofisi ya DPP
- Uharibifu unavyotishia uoto wa miombo Tanzania
- VIDEO: Uhasama wa Makamba, Mgeja wafikia mwisho
"Hongera nyingi kwa Tanzania kwa hatua hii nyingine ya kuongeza ndege mpya, " amesema Sameer.
Naye mkurugenzi mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema, “baada ya ununuzi wa ndege hii mpya kukamilika tutakuwa na ndege tano ndogo ambazo zitatumika kutoa huduma za usafiri wa anga nchini na nchi za jirani.”
Amesema shirika hilo litaendelea kuboresha huduma zake kwa kuzifanyia kazi kero wanazokumbana nazo wateja zikiwamo kuchelewa na kusitishwa kwa safari za ndege.