Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Minja aeleza vikwazo vya biashara nchini

Video Archive
Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Johnson Minja amesema ili Tanzania kuwa na uchumi wa kati mwaka 2025, Serikali inapaswa kuondoa vikwazo vya kibiashara vilivyopo.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumatatu Juni 11, 2018 Minja amevitaja vikwazo hivyo kuwa ni kodi zisizo rafiki, sera zisizotabirika na urasimu wa kukamilisha utaratibu wa kuanzisha na kuendesha biashara.

Minja ametoa kauli hiyo alipotembelea ofisi za gazeti la Mwananchi zilizopo Tabata Relini jijini hapa.

Amesema endapo changamoto hizo zitatafutiwa ufumbuzi kasi ya ukuaji uchumi itaenda juu zaidi.

“Ili kuweza kufikia uchumi wa kipato cha kati, Serikali inapaswa kuweka sera zinazotabirika ili kuvutia wawekezaji zaidi,” amesema Minja.

Pia, amependekeza  mamlaka mbalimbali zinazosimamia ubora wa bidhaa kupunguza tozo na kuangalia namna ya kupanua wigo wa ukusanyaji kodi ili kupunguza rundo la kodi kwa watu wachache.

Amebainisha kuwa jambo hilo litavutia uwekezaji zaidi hivyo kuchangia kukua kwa uchumi akisisitiza, “imetosha, ugumu wanaoupata walipa kodi wachache waliopo ufike mwisho. Tuwape mapumziko sasa.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz