Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Hali ilivyo Karume, mabomu ya machozi yarindima

Video Archive
Mon, 17 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi mkoani Dar es Salaam wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara wa soko la Karume (Mchikichini) ambao wameandamana na kufunga barabara iliyopo karibu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Amos Makalla wakishinikiza kuruhusiwa kuendelea na biashara katika soko hilo lililoungua usiku wa kuamkia jana Jumapili.

Polisi mkoani Dar es Salaam wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara wa soko la Karume (Mchikichini) ambao wameandamana na kufunga barabara iliyopo karibu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Amos Makalla wakishinikiza kuruhusiwa kuendelea na biashara katika soko hilo lililoungua usiku wa kuamkia jana Jumapili. Wafanyabiashara hao maarufu machinga wamefunga barabara hiyo muda mfupi baada ya kuandamana mpaka kwenye geti la kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam huku wakidai kuwa wanataka RC Makalla atoe tamko la kuwaruhusu waendelee kufanya shughuli zao kwenye soko hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live