Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utumbo wa kitabu waadimika sokoni, wachina watajwa

Utumbo Kitabu Utumbo wa kitabu waadimika sokoni, wachina watajwa

Fri, 26 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UTUMBO wa aina ya kitabu umetajwa kuadimika katika maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na upatikanaji wake kuwa mgumu kwenye machinjio na kusababisha bei kupanda.

Kuadimika huko kunadaiwa kusababishwa na raia wa China kununua kwa wingi bidhaa hiyo kutoka katika machinjio na kuusafirisha utumbo huo kwenda nchini mwao.

HabariLEO imebaini hayo baada ya kufanya uchunguzi kwa zaidi ya mwezi mmoja kwenye machinjio, maduka ya kuuza nyama na kwa wafanyabiashara wa chakula.

Akizungumza , mfanyabiashara wa chakula Tazara wilayani Temeke, Fidolin Francis alisema bei ya utumbo imepanda ikilinganishwa na miezi minne iliyopita ambako kilo 10 za utumbo ambazo zinakuwa na aina mbalimbali za utumbo, ilikuwa inauzwa Sh 40,000 lakini sasa inauzwa Sh 60,000.

Francis alisema katika kifurushi hicho, utumbo wa kitabu unakuwa umekosekana au ukiwapo unakuwa mchache sana, na kuwa anadhani uhitaji wake umekuwa mkubwa zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live