Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufafanuzi: Sheria inaruhusu Serikali kukopa BoT

BoT Yatoa Kanuni Za Maduka Ya Kubadilishia Fedha Za Kigeni 2023 Ufafanuzi: Sheria inaruhusu Serikali kukopa BoT

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema kuwa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006 Sura ya 197 inatoa nguvu kwa Serikali kuchukua mkopo wa muda mfupi wa mpaka asilimia 18 ya mapato ya Serikali kupitia akaunti zake zilizopo Benki Kuu.

Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki kutoka BoT, Agathon Kipandula amesema mkopo huo hutolewa pale ambapo Serikali ina dharura, ili kuziba nakisi iliyopo ambapo kiasi hicho cha fedha hurudishwa ndani ya siku 180.

Amesema utaratibu huo ni wa kawaida na hufanyika kwa benki kuu za nchi nyingi duniani pindi Serikali inapohitaji fedha za kugharamia bajeti wakati bado inaendelea kujipanga na kukusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali.

Hivi karibuni kupita mtandao wa X, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba alichapisha taarifa ikisena kuwa Serikali kukopa Benki Kuu ni jambo la kawaida na huwa linafanyika kila mwaka kutokana na Sheria ya BoT inayoruhusu kutoa mkopo wa muda mfupi kwa Serikali ili kukidhi mahitaji ya matumizi ambayo yanakuwa hayajapata mapato.

Taarifa hiyo ya Waziri Nchemba iliweka bayana kuwa kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023, Serikali ilikuwa inaweza kukopa BoT kiasi kinachofikia shilingi Trilioni 4.5.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live