Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tundu: Nikichaguliwa wakulima wa pamba hawatakopwa

11f144b617552c2a69c49eeb49bf197d Tundu: Nikichaguliwa wakulima wa pamba hawatakopwa

Thu, 3 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema andapo achaguliwa, serikali yake itaondoa kasumba ya wakulima wa pamba kukopwa mazao yao.

Aliyasema hayo Ilemela jijini Mwanza na kuahidi kuwa Serikali atakayoiunda italinda maslahi ya wavuvi na wakulima wa pamba katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Lissu alisema akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania atahakikisha hakuna mkulima wa pamba atakayekopwa mazao yake na kwamba, kutakuwa na utaratibu wa kununulia mazao yao kwa fedha taslimu.

Aliyasema hao katika uwanja wa Furahisha akiwa na mgombea mwenza wake, Salum Mwalimu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe na wagombea ubunge kupitia chama hicho.

Lissu alisema akichaguliwa, Serikali ya Chadema itajenga maduka makubwa katika vituo vya mabasi kwa ajili ya kuwakodishia wafanyabiashara watakaokuwa wanalipa kidogo kidogo.

Aidha, alisema akichaguliwa serikali atakayoiunda itaboresha maslahi ya watumishi wakiwemo polisi, wauguzi na madaktari.

Aliahidi pia kuimarisha upatikanaji ajira hasa kwa vijana ha;li itakayotokana na ukuaji, uimarishaji uchumi na kwamba, atajenga mfumo wa huduma za bima kwa wote ili kila Mtanzania apate tiba stahiki kwa gharama nafuu.

Nye Mgombea Mwenza wa Chadema, Mwalimu, aliwaomba wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kumchagua Lissu kwa madai kuwa, anajua changamoto zinazowakabili Watanzania.

“Mimi kama mgombea mwenza wake, nimejiandaa kimwili na kiroho kumnadi Tundu Lissu na kumsaidia pindi atakapochaguliwa kuwa Rais wa nchi," alisema.

Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika aliomba Watanzania wamchague Lissu awe Rais wa Tanzania kwa kuwa ni suluhisho la shida za Watanzania ukiwemo ukosefu wa ajira.

Chanzo: habarileo.co.tz