Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Teknolojia hii kusaidia wakulima wa miwa kukabili uhaba wa miwa

MIWA (600 X 337) Teknolojia hii kusaidia wakulima wa miwa kukabili uhaba wa miwa

Fri, 13 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kuongeza ufanisi na kuondokana na uhaba wa sukari nchini wakulima wa miwa watapata fursa ya kunufaika na ubunifu na teknolojia za kisasa za kilimo zitakazooneshwa kupitia maonesho ya Siku ya Wakulima wa Miwa Kilombero.

Maonesho hayo yanayotarajiwa kufanyika kwa siku tatu katika Bonde la Kilombero yataanza Oktoba 10 hadi 12, 2024 kwa lengo la kuwawezesha wakulima kujua teknolojia za kisasa zinazolenga kuongeza uzalishaji, ufanisi, na kujitegemea katika sekta ya sukari.

Kwa mara ya kwanza maonesho ya mwaka huu yanafanyika kwa siku tatu ambapo yanatarajiwa kuvutia maelfu ya wakulima wa miwa na wadau wa sekta ya kilimo.

Teknolojia mbalimbali, zikiwemo vifaa vya kilimo, mifumo endelevu ya umwagiliaji na mashine za kisasa zitaoneshwa ili kusaidia wakulima kuongeza mavuno na kupunguza athari za kimazingira na gharama za uendeshaji.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi naMeneja Mawasiliano na Mahusiano na Wadau wa Kampuni ya Sukari Kilombero, Victor Byemelwa amesema lengo kubwa la maonesho hayo ni kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji.

"Tumeongeza muda wa maonesho ya wakulima wa miwa Kilombero mwaka huu ili wakulima wapate fursa ya kuona ubunifu na teknolojia za hali ya juu zinavyobadili sekta ya miwa. Teknolojia hizi zitawezesha wakulima kuongeza uzalishaji, kuboresha ufanisi, na kuifanya Tanzania kujitegemea katika uzalishaji wasukari,” amesema Byemelwa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live