Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania na Comoro kuimarisha ushirikiano maeneo manne

Tanzania Na Comoro Kuimarisha Ushirikiano Maeneo Manne.png Tanzania na Comoro kuimarisha ushirikiano maeneo manne

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania na Visiwa vya Comoro zimesaini Hati nne za makubaliano kwenye kilele cha mkutano wa kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Comoro uliofanyika Julai 24, 2024 jijini Dar es Salaam.

Hati zilizosainiwa katika kikao hicho zinazojumuisha nyanja za ushirikiano wa kidiplomasia, afya, biashara na viwanda pamoja na teknolojia ya habari.

Utiaji saini hati hizo umeshuhudiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro anayeshughulikia nchi za Kiarabu, nchi zinazozungumza Kifaransa, diaspora na utangamano wa Afrika, Mohamed Mbae.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa kihistoria, Waziri Tax ameelezea umuhimu wa kusainiwa kwa hati hizo kuwa itawezesha pande hizo mbili kuwa na ushirikiano ulio katika mpangilio mzuri katika nyanja husika na hivyo kuleta tija zaidi.

"Pamoja na kutia saini hati za Makubaliano pia tumekubaliana kuendelea kushirikiana katika maeneo mengine mengi ikiwemo miondombinu, nishati, ulinzi na usalama, uchumi wa buluu, utalii, utamaduni, sanaa na michezo na maendeleo ya vijana," ameeleza Dk Tax.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live