Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA: Mgomo wa Namanga umemalizika

Mgomo Tenma Malori Polisi TRA: Mgomo wa Namanga umemalizika

Fri, 26 Jul 2024 Chanzo: Mwananchi

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo July 26,2024 imetoa taarifa kwa Wateja wake, Wananchi na Wanajumuiya Wote wa Afrika ya Mashariki kuwa mgomo wa Mawakala wa Forodha na Ushuru wa bidhaa katika Mpaka wa Namanga umemalizika na shughuli zinaendelea Kama kawaida.

TRA imesema mgomo huo umemamlizika kutokana na kikao kilichofanyika kati ya Maofisa wa Forodha na Mawakala kupata ufumbuzi wa changamoto zilizokuwa zimetolewa awaliā€¯

Itakumbukwa @AyoTV_ jana iliripoti kuwa Mawakala wa Forodha pamoja na Wasafirishaji wenye magari zaidi ya 500 wa Tanzania walifanya mgomo ikiwa ni siku ya pili katika mpaka wa Namanga uliopo katika Wilaya ya Longido Mkoani Arusha wakishinikiza kupunguzwa kwa utitiri wa kodi pamoja kutokea kwa sintofahamu kwenye mashine za EFD kwa Wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa kwenda nje ya Nchi.

Makamu Mwenyekiti wa Forodha katika mpaka wa Namanga, Alois Makyao aliiambia Ayo TV kuwa wamesitisha usafirishaji na kuomba mfumo kuwekwa sawa ikiwemo ucheleweshaji wa ukaguzi na kusema magari zaidi ya 500 yameshindwa kwenda Kenya baada ya mgomo huo na kuiomba Serikali kuingilia jambo hilo kwa kuwa Serikali pamoja na Wafanyabiashara hao wanapoteza mapato kwa wap kuendelea kukaa hapo mpakani ambapo baada ya ripoti hiyo TRA wamefanya nao kikao na kumaliza mgomo huo.

Chanzo: Mwananchi