Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPSF kumpata mrithi wa Mengi Agosti 28

13547 TPSF+PIC TanzaniaWeb

Fri, 24 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), imesema Mwenyekiti mpya wa taasisi hiyo atapatikana Agosti 28 mwaka huu baada ya  Mwenyekiti aliyepo kwa sasa Reginald Mengi kumaliza muda wake.

Mchakato wa kumpata mrithi wa nafasi hiyo utafanyika kupitia Mkutano Mkuu wa TPSF, utakaofanyika kwa siku mbili, kuanzia Agosti 27 hadi 28, mwaka huu.

Pamoja na mchakato wa kumpata mrithi wa nafasi hiyo, mkutano huo pia utakuwa na ajenda mbalimbali kujadili tuhuma za rushwa dhidi ya wafanyabiashara nchini.

Akizungumza na wanahabari leo Agosti 23, 2018, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Godfrey Simbeye amesema mkutano huo utaangalia pia uwezekano wa kuandaa kanuni za maadili kwa wanachama na wafanyabiashara nchini.

"Kumekuwa na malalamiko sana hususani katika sekta ya ujenzi, malalamiko ya rushwa, sekta binafsi inalalamikiwa kuwapo kwa udanganyifu, madai ya kutoamiana kati ya serikali na sekta binafsi katika ulipaji kodi, tunataka tumalize malalamiko haya, "amesema Simbeye.

Chanzo: mwananchi.co.tz