Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TIC yasaka wawekezaji wazawa

Uchumi Kupanda TIC yasaka wawekezaji wazawa

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kimeanza kampeni kuhamasisha uwekezaji wa ndani, lengo likiwa ni kuhakikisha Watanzania wanazijua fursa za uwekezaji na kujipatia vipato ili kuondokana na umaskini.

Akizungumza Januari 10, 2024 Mjini Geita baada ya kutembelea wawekezaji wazawa, Mkurugenzi wa TIC, Gilead Teri amesema kampeni hiyo ina malengo mawili.

“Kwanza ni kuwaonyesha Watanzania kuwa, kuna wazawa wamewekeza na kupata manufaa; pili kuwaeleza fursa wanazoweza kuzipata kupitia kituo cha uwekezaji,” amesema.

Teri amesema Serikali imerahisisha uwekezaji kwa wazawa kwa kuweka sheria inayorahisisha uwekezaji, ikiwamo kupunguza kiwango mwekezaji mzawa kutoka Dola 100, 000 za Marekani za awali hadi kufikia Dola 50,000 za Marekani.

Mkurugenzi huyo amesema Sheria imeweka vivutio vya uwekezaji lengo likiwa ni kulinda uwekezaji wa ndani huku kivutio kimoja ni msamaha wa kikodi kwa baadhi ya vifaa kuondolewa ushuru kwa asilimia 75 hadi 100.

Akizungumzia ukuaji wa sekta ya uwekezaji nchini, Teri amesema sekta hiyo imekuwa kwa zaidi ya asilimia 60 kutoka mwaka 2022 hadi 2023.

Na kwa mwaka 2023 miradi 504 yenye mitaji ya thamani ya dola 5.6 bilioni ilisajiliwa ikilinganishwa na miradi 272 yenye thamani ya Dola 300 milioni za Marekani iliyosajiliwa mwaka 2022.

Amesema katika miradi iliyoongezeka nusu yake ni miradi ya wazawa ambayo mingi ni ya sekta za kilimo, uchukuzi, viwanda, madini na utalii.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Cornel Magembe amesema Mkoa wa Geita una fursa nyingi za kuwekeza zikiwamo sekta za utalii, kilimo na uwekezaji kwenye sekta ya mifugo ile ya madini.

Mwekezaji mzawa Attanas Inyasi anayemiliki kampuni ya usafirishaji ya Blue Coast amesema misamaha ya kodi inayotolewa kwa wawekezaji imemsaidia kukuza biashara yake na na kutoa ajira kwa Watanzania wengine.

Amewataka Watanzania kujenga uthubutu na kufanya biashara badala ya kuogopa kwa kuwa uwekezaji wa sasa unahitaji na umerahisishwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live