Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TIC: Wawekezaji wengi wanatakiwa wawe Watanzania

FEDHA WEB TIC: Wawekezaji wengi wanatakiwa wawe Watanzania

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

"Ilikuwa ukionekana Mtanzania unataka kuwekeza sehemu fulani, watu wanasema hivi mwenzetu huyu anaweza kuwa mwekezaji kweli? Na wakati mwingine watu walikuwa wanaamini kwamba mwenye uwezo wa kufanya hivyo lazima awe anatokea nje.

"Lakini kampeni hii ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani imelenga kutujulisha sote kwamba hivyo sivyo. Kuna wawekezaji wengi wenye uwezo na weledi stahili ndani ya nchi ambapo kimsingi ndio wanatakiwa kuwa sehemu kubwa ya wawekezaji."

Hayo ni maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi aliyosema wakati wa semina iliyoendeshwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa wawekezaji wa ndani mkoani hapa.

Huu ni mwendelezo wa kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani inayoendelea Kanda ya Ziwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live