Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TASAC yataka punguzo la kodi boti za wavuvi

Uvuvi Ziwa Tanganyika.jpeg TASAC yataka punguzo la kodi boti za wavuvi

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), imeshauri kupunguzwa kwa kodi za malighafi za kukarabati boti za wavuvi, ili kuongeza ufanisi wake.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TASAC, Nahodha Mussa Mandia jana Julai 24, 2024 akiwa ziarani katika Bandari ya Bagamoyo kukagua ufanisi na miundombinu ya bandari hiyo na kutembelea mwalo wa Kaole na Chuo cha Uvuvi Mbegani.

Mohamed Mwinyijuma ambaye ni mvuvi wa kutumia boti, amesema gharama za vifaa vya ukarabati ni kikwazo kwao katika ufanyaji wa kazi boti inapoharibika.

"Gharama za ujenzi wa boti za faiba (fibre materials) zipo juu, tunaomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ipunguze kodi," amesema Mwinyujuma.

Sensa ya Mwaka 2022 imeonyesha kuwa Tanzania ina jumla ya vyombo vidogo 52,189 vinavyofanya shughuli za uvuvi na usafirishaji wa abiria na mizigo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live