Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatangaza mwelekeo mpya wa madini

Mud Matope Madini Serikali yatangaza mwelekeo mpya wa madini

Wed, 16 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema mpango wa Serikali kwa sasa ni kuimarisha taarifa na mchakato wa upatikanaji wa madini ya kimkakati, kwa kuwa hivi sasa dunia imehamia katika matumizi ya nishati safi, na kwamba ifikapo mwaka 2050 mahitaji ya madini ya kimkakati yataongezeka kwa asilimia 150.

Akizungumza katika mdahalo uliofanyika kwa njia ya mtandao wa Zoom, Mavunde amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na madini mengi ya kimkakati ambayo yanahitajika duniani kwa ajili ya nishati safi.

Ametaja madini hayo ya kimakakati yaliyopo nchini kuwa ni pamoja na Nickel, Copper, Cobalt, Manganese, Vanadium, Lithium na Graphite (kinywe).

Waziri Mavunde amesema hivi sasa Tanzania inajipanga kuwa mmoja kati ya wazalishaji wakubwa wa madini ya kimkakati barani Afrika.

Ametolea mfano madini ya Kinywe ambayo mahitaji yake duniani hivi sasa ni tani Milioni 6.5 kwa mwaka na uzalishaji wa dunia hivi sasa ni tani Milioni 1.2 huku China ikiongoza kwa kuzalisha asilimia 64 na kwa Afrika nchi ya kwanza ni Madagascar (13%) ya pili Msumbiji (10%) na ya tatu ni Tanzania ikizalisha kwa asilimia 0.6.

Ili kufikia lengo la kuwa moja ya wazalishaji wakubwa, Waziri Mavunde amesema ipo miradi mikubwa 12 inayokwenda kuanza hivi karibuni na miradi mingine ambayo tayari imeshaanza kama ule uliopo Mahenge (Morogoro) na Ruagwa (Lindi) ambayo inazalisha madini ya Kinywe (Graphite).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live