Serikali ya Tanzania ina mpango wa kujenga matenki 15 ya kuhifadhi mafuta Kigamboni ambapo mradi huo utagharimu Sh678 bilioni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 12, 2024 baada ya kutembelea ujenzi huo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema kati ya matanki hayo 6 yatakuwa ya dizeli, 5 petroni na matatu yatakuwa ya gesi.
Amesema mradi huo unaenda kutekelezwa kwa miaka miwili huku ukisimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA, kwa kushirikiana na wakandarasi;
"Tunafahamu mwa sasa meli za mafuta zinachukua muda mrefu katika kuleta mafuta hii inatokana na upungufu wa matenki yaliyopo nchini pia mafuta hayo yakitolewa yanapelekwa kwenye vituo husika na kama Serikali tumeamua kujenga matenki ili yawekewe mafuta na kupelekea wateja wetu," amesema Profesa Mbarawa.
Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Hamis Hassani amesema mradi huo utapunguza kero ya mafuta ikiwemo bandarini na utamalizika katika muda uliopangwa.