Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sera zavutia wawekezaji Tanzania

Polish 20240628 145257170 Sera zavutia wawekezaji Tanzania

Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sera nzuri za kibiashara zilizowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imewezesha kampuni mbalimbali za Kitanzania kuanzisha na kutengeneza bidhaa zao wenyewe. - Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ZAC, Samwel Ngowi na kueleza kuwa mazingira ya biashara nchini ni mazuri kwa kuwa kampuni zinaweza kuuza kwa urahisi bidhaa zao nje ya nchi.

Amesema Kampuni ya ZAC inazalisha bidhaa zake nje ya nchi, kisha kuzisambaza hapa nchini, imejikita katika uzalishaji wa vifaa vya umeme vya kielektroniki vya nyumbani, simu za mkononi pamoja na vifaa vya simu.

Amesema, kampuni hiyo ina maduka nchini Zambia huku kwa hapa nchini ikiwa na maduka yake Mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Moshi, Mwanza, Morogoro, Singida na Dodoma.

“ZAC imekuwa sokoni tangu Juni 2020 ikipania kuwa msambazaji mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, huku likiwa ni kutengeneza ajira kwa vijana wa Kitanzania katika nyanja tofauti kama vile mauzo na masoko," amesema. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live