Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta ya madini yaleta bilioni 247/-

Madini Pic Data Sekta ya madini yaleta bilioni 247/-

Wed, 16 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde amesema serikali imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 287 katika kipindi cha robo ya kwanza, ikivuka lengo la awali la makusanyo ya shilingi bilioni 247 katika sekta ya madini.

Akizungumza wakati wa mjadala wa mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika uboreshaji wa sekta madini nchini uliofanyika kwa njia ya mtandao, Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema serikali ya awamu ya sita imeendelea kuweka usimamizi mzuri wa masoko ya madini ambayo imesaidia kudhibiti utoroshaji wa madini nchini .

“Masoko ya madini yamekuwa na mchango mkubwa katika kudhibiti utoroshaji wa madini na hii imesaidia kuongeza mapato ya serikali,” alisema Mavunde.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live