Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni aibu miradi ya Serikali kutokidhi viwango

Kilimo House Ni aibu miradi ya Serikali kutokidhi viwango

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa amewataka wahandisi na watumishi wa tume hiyo kuheshimu, kusimamia na kutekeleza miradi ya umwagiliaji kwa viwango na ubora.

Amesema ni aibu kwa taasisi kuwa na miradi isiyokidhi viwango, hivyo ni muhimu usimamizi wake ukazingatia matokeo yenye ubora kwani hatakuwa tayari kuona miradi hiyo inaiangusha Serikali.

Mndolwa amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa kikao kazi na menejimenti, wasimamizi wa miradi, wahandisi wa mikoa, wahakiki ubora wa miradi na baadhi ya watumishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live