Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege zashindwa kupaa Marekani, safari zasitishwa

Delta Airlines Ndege zashindwa kupaa Marekani, safari zasitishwa

Fri, 19 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Safari zote za ndege katika Mashirika kadhaa makubwa ya ndege ya Marekani ikiwemo Delta, United na American Airlines zimesitishwa leo Ijumaa asubuhi (Julai 19, 2024) kutokana na tatizo la teknolojia lililokumba sio tu Mashirika ya Ndege Marekani bali hata Viwanja vya Ndege, Mabenki na Mashirika ya Utangazaji ya Ulaya na Nchi mbalimbali ikiwemo Australia.

Baadhi ya Vyombo vya habari vimeripoti kuwa huenda jaribio la Kampuni ya usalama wa mtandao ya Crowdstrike kufanya marekebisho katika programu zinazotumika sehemu mbalimbali duniani likawa ni sehemu ya vyanzo vya kompyuta kuvurugwa na kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa.

Tatizo hili limesababisha Viwanja vya ndege sio tu vya Marekani bali hata Uingereza na Nchi nyingine kadhaa kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa na kupelekea baadhi ya safari za ndege kusitishwa huku Uingereza wakisitisha hadi baadhi ya safari za treni.

Uwanja wa Ndege wa Berlin Nchini Ujerumani, Gatwrick Airport Nchini Uingereza, Melbourne Airport Nchini Australia ni sehemu ya Viwanja vilivyotangaza kuathirika na hitilafu hiyo ya kiteknolojia huku Google Cloud na Microsoft nao pia wakikiri kupitia changamoto hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live