Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwigulu, mawaziri wenzake wateta na Makamu wa Rais Benki ya Dunia

Mwigulu Na Mawaziri Wenzake Mwigulu, mawaziri wenzake wateta na Makamu wa Rais Benki ya Dunia

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba na Mawaziri wengine wamekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa.

Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki @AngellahKairuki, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa @JerrySilaa viongozi hao wamejadiliana masuala ya msingi ya kuendeleza ushirikiano.

Taarifa ya Wizara ya Fedha imesema majadiliano yalijikita katika kukuza ushirikiano katika eneo la uhifadhi na utalii pamoja na maendeleo ya watu na Taifa.

Bi. Kwakwa alisifu na kupongeza ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Benki hiyo na kwamba Tanzania imekuwa nchi inayofanya vizuri kiuchumi kati ya nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na ni mnufaika mkubwa wa programu mbalimbali zinazoendeshwa na Shirika hilo kubwa la Fedha duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live