Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema kuwa miongoni mwa changamoto kubwa inayoikabili Taifa lake ni wananchi kujikita zaidi kwenye kilimo cha tumbo badala ya kuwekeza katika kilimo cha biashara ambacho kinaleta ajira na utajiri.
Submitted by Agnes Kibona on Alhamisi , 20th Mei , 2021 Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Kauli hiyo ameitoa leo Mei 20, 2021, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza mara baada ya kutiliana saini mkataba wa tano wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi mkoani Tanga na Rais Samia Suluhu Hassan, na kusisitiza kwamba wasijikite zaidi na sekta ya ICT na mafuta badala yake wajiwekeze pia kwenye kilimo chenye tija.
"Ukijiuliza utajiri na ajira vinatoka sekta gani ni kilimo cha biashara, kwetu watu wamelala wanafanya kilimo cha tumbo pekee, mtu anakuwa hapo miaka 80 ya uhai anafanya kilimo cha tumbo peke yake huu ni ugonjwa mkubwa sana kule Uganda", amesema Rais Museveni
Tazama video hapa chini