Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde: Masoko ya madini yaanza kuleta faida

Mavunde Anthony Zzz Mavunde: Masoko ya madini yaanza kuleta faida

Wed, 16 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema Serikali imeimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato na kudhibiti utoroshaji wa madini ili nchi iweze kunufaika na mapato yatokanayo na kodi, tozo na ushuru wa madini.

Akizungumza katika mdahalo uliofanyika kwa njia ya mtandao wa Zoom Waziri Mavunde amesema hatua ambazo Serikali imeendelea kuzichukua zimeanza kuzaa matunda, hasa ile ya kuanzisha masoko ya madini ambayo yameanza kuleta faida.

Amesema kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016 jumla ya fedha zilizokusanywa kwenye maduhuhi ni shilingi Bilioni 161 ambazo ziliingia kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

Waziri Mavunde ameongeza kuwa kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 sekta ya madini imeingiza katika Mfuko Mkuu wa Serikali zaidi ya shilingi Bilioni 753 na mafanikio hayo yametokana na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko ya madini, biashara ya madini kupitia katika mifumo rasmi na kudhibitiwa kwa utoroshaji wa madini.

Kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 sekta ya madini imewekewa lengo la kukusanya shilingi Trilioni moja, na kwa siku 90 za mwanzo zimekusanywa shilingi Bilioni 287.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live