Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani kuipa adhabu kampuni ya Boeing - Mwanasheria

Marekani Kuipa Kampuni Ya Ndege Ya Boeing 'adhabu Ndogo'   Mwanasheria.png Marekani kuipa kampuni ya ndege ya Boeing 'adhabu ndogo' - Mwanasheria

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Wakili anayewakilisha waathiriwa wa ajali mbili mbaya za ndege aina ya Boeing 737 Max ameambia BBC kwamba serikali ya Marekani inapanga kuipa kampuni hiyo "adhabu ndogo".

Paul Cassell, ambaye anasema alipata taarifa "moja kwa moja kutoka kwa Wizara ya Sheria", aliongeza kuwa mpango huo unajumuisha faini ndogo, miaka mitatu ya kuchunguzwa tabia na ukaguzi huru wa usalama.

Boeing haikujibu mara moja ombi la BBC la kutoa maoni yake, huku Wizara ya Sheria ikikataa kutoa taarifa.

Wiki iliyopita, waendesha mashtaka wa Marekani walipendekeza kwamba Wizara ya Sheria ifungue mashtaka ya jinai dhidi ya mtengenezaji huyo wa ndege.

Hiyo ilikuwa baada ya wizara hiyo kusema kampuni ya Boeing ilikiuka suluhu la mwaka 2021 kuhusiana na ajali ambazo ziliua watu 346.

"Kumbukumbu ya watu 346 wasio na hatia waliouawa na ndege aina ya Boeing inadai haki zaidi kuliko hii," alisema Bw Cassell, akiongeza kuwa "familia zitapinga vikali adhabu hii".

Ajali za ndege hiyo - zote zikihusisha ndege aina ya Boeing 737 Max - zilitokea ndani ya miezi sita ya kila mmoja.

Ajali iliyohusisha Lion Air ya Indonesia ilitokea Oktoba 2018, ikifuatiwa na ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia iliyotokea Machi 2019.

Chanzo: Bbc