Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapato soko la feri yapaa

FEDHA WEB Mapato soko la feri yapaa

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Soko la Kimataifa la Samaki Ferry Jijini Dar es Salaam, Abdallah Mfinanga amesema mapato ya soko hilo yameongezeka kutoka wastani wa shilingi milioni 118 kwa mwezi hadi kufikia shilingi milioni 155 kwa mwezi, hususani tangu achukue uongozi kuanzia Juni 2023 hadi hesabu za leo Julai Mosi 2024.

Mfinanga amesema mapato hayo yameongezeka kutokana juhudi za kusimamia mapato kikamilifu.

"Soko hili ni moja ya chanzo cha mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo kiasi cha fedha huenda halmashauri na kinachobaki ni kwa ajili ya matumizi na shughuli za soko," amesema Mfinanga.

Katika hatua nyingine, Mfinanga amesema kuwa soko hilo linapokea samaki kutoka maeneo mbalimbali ya bahari ya Hindi pamoja na Ziwa Victoria, na kwamba lina zaidi ya zone nane. Amesema soko pia linahudumia watalii takribani 12,000 wakiwemo Wachina.

Mfinanga amesema soko hilo lipo mbioni kuboreshwa ikiwa ni pamoja na kujengwa fremu za maduka 42 karibu na kituo cha mabasi ya mwendokasi cha Magogoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live