Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maneno ya Kusaga kwa mkewe, Mwanae "Wangetumia vizuri au vibaya" (Video+)

Video Archive
Sat, 7 Aug 2021 Chanzo: millardayo.com

NI Agosti 6, 2021 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akizungumza mbele ya wageni kuhusu sababu za kuanzisha mchongo wa ‘Big Joe’ utakaosaidia vijana 55 ili wakajiendeleze katika Biashara zao.

Joseph Kusaga leo ametoa mchongo kwa Vijana 55 wa shilingi Milioni 550 ili tu waweze kukuza biashara zao.

“Kama Mungu amekupa nafasi ya kuwa mahali fulani itumie na kuwasaidia wengine, lakini mimi namshukuru Mungu kwa nafasi niliyoipata naweza tena kusema wengine wangepata nafasi hii wangeitumia vizuri ama vibaya“- Joseph Kusaga

“Nilisema kwamba ni lazima nihakikishe kwamba natoa nafasi iwezekanavyo kwa vijana wengi sana wapate nafasi ya kujiendeleza katika maisha yao, kwahiyo Vijana waliojitokeza ni wengi walikuwa wanafika Elfu moja lakini nawashukuru Fauzia, Reuben kwa kufanikisha kupata vijana 55″-Joseph Kusaga

“Na Vijana waliopata huu mchongo wa Big Joe pia msiwasahau Vijana wengine mkawashike mkono na kuwasaidia ili watimize ndoto zao”- Joseph Kusaga

Chanzo: millardayo.com