Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa awatuliza wakulima wa pamba

76690 Majaliwa1+pic

Sun, 22 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Chato. Waziri Mkuu nchini Tanzania, Kassim Majaliwa amesema wakulima wote waliouza pamba katika vyama vya ushirika watalipwa fedha zao.

Akizungumza  leo Jumamosi Septemba 21, 2019 na wakulima wa zao hilo katika kiwanda cha pamba wilayani Chato, Majaliwa amesema kutokana na bei ya pamba kushuka katika soko la dunia, wanunuzi wanashindwa kununua.

Amesema Serikali imeingilia kati na kuruhusu wachukue fedha benki ili pamba yote inayonunuliwa kwa wakulima iweze kulipwa.

Amesema awali walitarajia kuvuna kilo 250,000 za lakini hadi sasa kilo 350,000 zimekusanywa na bado nyingine zipo kwa wakulima zinaendelea kukusanywa.

Amesema kutokana na maghala ya wanunuzi wa pamba kujaa, Serikali imelazimika kutafuta maghala jijini Dar es Salaam ili kuzihifadhi na kuendelea kutoa pamba kwa wakulima hadi pale bei itakapokua nzuri katika soko la dunia.

Ametoa wito kwa wafanyabiashara nchini kujenga viwanda vya kusokota nyuzi na kutengeneza nguo ili kuliwezesha zao hilo kuwa na thamani kubwa zaidi, kwamba Serikali ipo tayari kumsaidia mwekezaji atakayejenga kiwanda cha nguo.

Pia Soma

Advertisement
 

Chanzo: mwananchi.co.tz