Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa awataka wawekezaji wasiogope kukopa

28245 Pic+majaliwa+kopa TanzaniaWeb

Thu, 22 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wawekezaji nchini kutoogopa kukopa kwenye mabenki kwani ndiyo fursa nzuri ya kupiga hatua.

Akizungumza mjini Tabora wakati wa Jukwaa la Fursa za biashara na uwekezaji, amesema hakuna haja ya kuulizia kuhusu mitaji kwani mabenki yapo yanakopesha na kutoa mfano wa NMB kutenga Sh500bilioni kwa ajili ya kukopesha.

Pia ametaka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania nayo kutumiwa kwa maendeleo ya kilimo.

Amesema ni muhimu kwa wawekezaji kuzitumia benki hizo huku akizitaka taasisi na mamlaka za Serikali  kuondokana  na urasimu ili wawekezaji wapate huduma haraka.

Amezitaka taasisi zinazohusiana kuwa na eneo moja ili wawekezaji waweze kuhudumiwa kwa haraka.

Kuwekeza Tabora ni faida kwani kuna usalama, uwanja wa ndege na barabara za uhakika huku kukiwa na ujio wa treni ya uhakika hivyo inafikika na inafaa kuwekeza.

“Ardhi ya kutosha na wilaya zimetenga maeneo ya uwekezaji huku hali ya hewa ikiwa nzuri, pia ni mzalishaji mzuri wa tumbaku na wilaya zimejiandaa kupokea wawekezaji,” amesema Waziri Mkuu.



Chanzo: mwananchi.co.tz