Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuacha kasumba iliyojengeka miongoni mwao kudhani kuwa kilimo cha zao la mkonge ni kwa ajili ya matajiri pekee.
Majaliwa amebainisha hayo leo alipotembelea Shamba la Mkonge la Kigombe lililopo wilayani Muheza mkoani Tanga kujionea ni namna gani linafanya kazi.
“Hapa wilayani Muheza kuna maeneo mazuri tu yanafaa kulimwa Mkonge naamini kuna watu walitaka kulima zao hili ila waliaminishwa kilimo hiki kinatakiwa kufanywa na watu wenye utajiri kitu ambacho sio kweli ” amesema Majaliwa.
Awali akizungumza katika tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amesema shamba hilo liimetoa ajira kwa wakazi wa mkoa huo na kwa mwezi serikali ukusanya kodi ya Shilingi milioni 90 na kusaidaia kuinua uchumi wa mkoa huo.