Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa awabana ma-RC kuhusu saruji

A44c01837e7b8461e1e06ec2986c59eb Majaliwa awabana ma-RC kuhusu saruji

Tue, 17 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ametoa siku nne kwa maofisa wa wizara yake na wakuu wa Mikoa kwenda katika viwanda vya uzalishaji saruji, kujua sababu za bidhaa hiyo kupanda ‘kienyeji’.

Amewataka maofisa hao kufika kwenye viwanda mbalimbali nchini Novemba 20, 2020, saa nne asubuhi, ili kupata maelezo kuhusu sababu za bidhaa hiyo kupanda sokoni.

Akizungumza mbele ya Rais John Magufuli baada ya kuapishwa kuwa Waziri Mkuu katika viwanja vya Ikulu, Chamwino jijini Dodoma, Waziri Majaliwa amehoji, sababu za bei ya saruji kupanda wakati Serikali haijapandisha kodi, makaa ya mawe wala kujafanya mabadiliko yoyote.

“Kuna upandaji wa saruji bila sababu za msingi, miaka mitano iliyopita tulijenga mazingira ya baiashara kuwa rahisi. Hatukutarajia saruji kupanda, mheshimiwa Rais naaanza na hilo.”amesema Majaliwa na kuongeza

“Tarehe 20 saa nne asubuhi, wakuu wa Mikoa yote waende kwenye viwanda kujua kwanini saruji imepanda wakati serikali haijapandisha kodi, makaa ya mawe. Tunahitaji maelezo kwanini bei ya saruji imepanda kwa kiasi hicho.

“Tulikuwa kwenye kampeni za uchaguzi watu wakajisahau wakadhani serikali haitafanya kitu,” amesema Majalia.

Waziri Majali amesema, kwa kuwa moja ya kazi yake kubwa ni kuhakikisha malengo ya Serikali na ilana ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2020 – 2025 inatimia, atapita kila wizara kusisitiza hilo.

“…nitapita kila wizara kuhakikisha mipango na ilani inatekelezwa, hilo ndio jukumu kubwa linaanza”

Pia, Waziri Majaliwa amewashukuru wabunge kwa kuridhia jina lake kuwa Waziri Mkuu akisema, tabia yake ni ile ile ya kuwasikiliza na kuwahudumia wabunge kwa maslahi ya Taifa.

“Nawashukuru wabunge wenzangu baadhi ya uthibitisho uliopelekwa bungeni, pia nashukuru kwa kunishindikiza. Ni matarajio yetu wakati wote tukiwa kwenye majukumu yetu tutatenda yale Watanzania wanatarajia.”

“Bado msimamo wangu ni ule ule wa kuwapokea, kuwasikiliza na kuwahudimia wabunge. Ni jukumu langu kuhakiklisha malengo yaliyowekwa na ilani ya uchaguzi yanakamilika,” amesema.

Mbali na Waziri Majaliwa kuapishwa, wengine walioapishwa ni Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pia Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha.

Baadhi ya wageni waliohudhulia ni; Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, Spika wa Bunge, Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.

Wengine ni; Maspika wastaafu; Pius Msekwa na Anne Makinda; Mawaziri wakuu wastaafu; John Malechela, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na Mizengo Pinda. Wakuu wote wa mikoa, makatibu wakuu wote wa wizara, wabunge wa Bunge la 12.

Chanzo: habarileo.co.tz