Wafanyabiashara wauzaji wa nafaka Chalinze mkoani Pwani, wameeleza ugumu wa upatikanaji wa zao la karanga kwa sasa sokoni kitu ambacho kinawafanya kupoteza wateja wao ambao wengi wao wanashindwa kununua karanga sababu ya bei kupanda ukitofautisha na awali.
Wakizungumza wafanyabiashara hao wanasema hapo awali bei ya karanga ilikuwa kilo moja ni shilingi 3,400 ila kwa sasa kilo ni shilingi 4,500 ambapo kwa upande wa kiroba ni shilingi 200,000 cha kilo hamsini, huku miezi miwili nyuma ilikuwa ni tsh 150,000 ambapo wamewataka wakulima kuendelea kuzalisha kwa wingi zao hilo.
"Biashara ya karanga sasa hivi imepanda sana iko juu, kilo tulikuwa tunauza elfu 3,400 sasa hivi tunauza elfu 4,500 kwahiyo kiroba kipo kwenye 200,000 cha kilo hamsini, hivyo wakulima wazalishe karanga kwa wingi ilituweze kuwa hudumia wananchi, amesema mmoja wa wafanyabiashara.
"Na sio kama sisi tunapenda kupandisha bei ila ni kutokana na uzalishaji na upatikanaji umekuwa changamoto hususani kwa kipindi hichi, shida sio kuzipata na hata zikipatikana zinapatikana kwa bei kubwa sana tofauti na zamani," amesema Bakari