Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya GF yaiomba serikali kuiunga mkono Hyundai kuwezesha kutengenezwa nchini

Samia Nyusi Sdac Kampuni ya GF yaiomba serikali kuiunga mkono Hyundai kuwezesha kutengenezwa nchini

Wed, 3 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wa maonyesho ya biashara ya kimataifa yakifunguliwa na mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi aliyeambatana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan walitembelea mabanda mbalimbali kabla ya kufungua na kutoa zawadi kwa washindi mbali mbali.

Akizungumza wakati Marais hao wakitembelea banda lao Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd , Imrani Karmali amesema baada ya ziara ya Rais nchini Korea kushawishi wawekezaji kuwekeza nchini wao kama GF Automobile, wamezungumza na wakorea na wako tayari kuja kuweka kiwanda cha kuunganisha magari ya Hyundai nchini.

Amesema wakorea hao walitaka lazima kuwe na oda kubwa kwa kuanzia sasa ambapo wao kupitia kiwanda chao cha kunganishia magari cha GFA wapo tayari kufanya hivyo.

“Ombi letu kwako mama tunaomba Serikali kupitia wizara na tasisi zake kutuunga mkono katika hili na matunda ya ziara yako nchini korea kuonekana kwa Hyundani kutengenezwa nchini Tanzania”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live