Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ifahamu hoteli ya ndege inayotamba Dubai

Dubais Five Hotel Launches Private Party Jet Ifahamu hoteli ya ndege inayotamba Dubai

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanasema sio kila mmoja anaweza kumiliki ndege binafsi lakini kuna uwezekano wengi zaidi wakalipia huduma za ndege hizo binafsi na kukidhi haja za mioyo yao, hicho ndicho kinachofanywa na Hoteli ya kifahari ya FIVE ya Dubai ambayo ilizindua Private Jet hii ya kifahari ambayo ina uwezo wa kupaa kwa saa 12 mfululizo angani.

Ni ndege ambayo Abiria wanaweza kufanya hadi party wakiwa angani na wanaposhikwa na njaa kuna jiko lililo na vifaa vyote vya kukarangiza chochote na meza (dinning table) inayomudu Watu nane ikiwa imeambatana na menu kutoka kwenye Hoteli inayomiliki Ndege hiyo aina ya ACJ 220, Airbus.

Ndege hiyo ambayo ndani ina chumba (Master Suite) chenye kitanda kikubwa cha kifahari na bafu lake, TV mbili za inch 55, WIFI yenye intanteti yenye kasi, inakodishwa kwa karibu dola elfu 15 kwa dakika 60 hivyo kwa atayetaka kupaa kwa saa 12 atalazimika kulipia karibu dola laki moja na elfu themanini (Tsh. milioni 480+).

Kampuni inayomiliki Ndege hiyo imeiambia CNN kuwa toka kuanzisha biashara hiyo April 2023, Ndege hiyo imekodishwa zaidi ya mara hamsini na Wateja wa VIP, Wakuu wa Nchi ambapo safari zilikuwa kati ya Ulaya, Marekani, Uingereza, Mashariki ya Kati, Afrika na Asia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live