Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndio nyama bora ya ngombe kwa biashara

Nyama Za Ng'ombe Hii ndio nyama bora ya ngombe kwa biashara

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amesema nyama bora inayopatikana nchini inatokea katikq mkoa huo kutokana na mazingira mazuri na rafiki ya ufugaji wa ng'ombe.

"Ng'ombe wanatunzwa na kukuzwa katika maeneo ambayo hayamtesi mnyama, ndio maana ukizunguka Tanzania yote ambayo wafugaji wanaenda, huwezi kukutana na mfugaji Mkurya au Mjita ndio maana wanakuwa huku, "

"Mazingira yenyewe hata Serengeti ambayo ndio mbuga yenye wanyama wengi duniani, hata haya maeneo (tunayoishi) yalikuwa ni maeneo ya wanyama na yalikuwa mazingira mazuri kwa wanyama ndio maana nyama inayotokea Mara ndio bora zaidi".

Kanali Mtambi amesema hayo wakati akiwakaribisha maafisa kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ambao wapo Kanda ya Ziwa kwenye muendelezo wa kampeni ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live