Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Biteko: Tunaendelea na maandalizi ya kuwauzia Umeme nchi za Jirani

Dkt Biteko Umeme Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko

Mon, 21 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema “Serikali inaendeleza vyanzo vipya vya Nishati, mfano; Umeme wa Jua, Upepo na Gesi, aidha kwasasa Asilimia 51 ya umeme unazalishwa kwa maji."

Ameongeza “Tanzania tumeendelea na maandalizi ya kuziuzia umeme nchi za Kenya, Rwanda, Burundi na sasa tunaendelea na mradi kwaajili ya kuunganisha na nchi ya Zambia, kupitia Umoja wa Mauzio ya Umeme wa pamoja katika nchi za Afrika Mashiriki na Jumuiya za Kusini mwa Afrika (SADC). Tuna Soko la uhakika na hivyo tunawakaribisha wawekezaji kuja kushirikiana nasi.”

Dkt. Biteko amesema hayo leo Oktoba 21, 2023 akiwa Nchini Singapore, wakati akishiriki katika mjadala kuhusu nishati, wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Kimataifa ya Nishati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live