Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DART kushusha mabasi 100 ya mwendokasi

Mwendokasi Msj DART kushusha mabasi 100 ya mwendokasi

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu, amesema katika jitihada za kuboresha uendeshaji wa mabasi ya mwendokasi benki ya NMB imekubali kutoa mkopo kwa Serikali ambayo inamiliki kampuni ya UDART kwa 85% ili kuongeza mabasi zaidi ya 100 ya mwendokasi.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo July 15,2024 katika Mkutano wa Msajili wa Hazina na Wahariri wa Vyombo vya habari, Mchechu amenukuliwa akisema “UDART sasa hivi ni kampuni inayomilikiwa 85% na Serikali, ilipoanza ilikuwa inaendeshwa na Sekta binafsi Serikali ilikuwa na mchango mdogo, tukajikuta ina madeni mengi, mabasi yake ndio hivyo, kwa miezi miwili nimekuwa nafanya vikao na DART kampuni inayosimamia miundombinu, na UDART inasimamia uendeshaji na mabasi.

“Tunaenda kuongeza idadi ya mabasi na kesho nina kikao na benki ya NMB ambayo ndio wanatukopesha, tutakuwa na kikao pale NMB na UDART, DART, LATRA kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa fedha wa kupata mabasi yasiyopungua mabasi 100 ambayo yataweza kutusaidia.

“La pili kwa hatua tuliyofikia tunahitaji kampuni zaidi ya tano au sita, sio kampuni moja tu ambayo siku wakigoma au kupata matatizo Mji wote umesimama, unapokuwa na Waendeshaji wengi pia ni rahisi kujua nani anatoa huduma nzuri.

“Tutahitaji miezi sita kuanzia tunapotoa oda mpaka mabasi yaje, tutafanya maongezi na NMB kesho tutajua lini mabasi yatakuwa yanafika, najua nitamuachia Mkurugenzi Mkuu wa UDART na Bodi yake kuisema kwa Umma lakini kazi yetu ni kuhakikisha wanapata pesa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live