Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya korosho yazidi kupaaa

Korosho 2aaz Bei ya korosho yazidi kupaaa

Fri, 11 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mnada wa kwanza wa korosho kwa msimu wa 2024/2025 umezinduliwa wilayani Newala mkoani Mtwara ukisimamiwa na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), huku bei ikipanda hadi kufikia shilingi 4,120 kwa kilo moja ya korosho ghafi kwa bei ya juu na shilingi 4,035 kwa bei ya chini.

Chama Kikuu cha Ushirika kinachohudumia wilaya za Newala na Tandahimba (TANECU) kilipeleka sokoni tani 3,857 za korosho katika mnada huo, ambazo zote zimenunuliwa.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mnada huo, ameeleza kuwa huo ni mwanzo mzuri ambao unaonesha kuwa msimu wa korosho wa 2024/2025 utakuwa wa manufaa kwa wakulima.

Amewakumbusha wakulima kuzingatia ubora wa korosho, hali ambayo itasaidia kuongeza thamani ya zao hilo katika minada inayofuata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live