Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AG Kilangi asema wakopeshaji binafsi kusimamiwa kisheria

27465 AG+PIC TanzaniaWeb

Sat, 17 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Adelardus Kilangi amesema Serikali imezingatia ushauri wa wabunge wa kuwaingiza wakopeshaji binafsi (mtu mmoja mmoja) katika usimamizi wa Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018.

Akichangia muswada huo bungeni leo Ijumaa Novemba 16, 2018, Dk Kilangi amesema wabunge katika michango yao walisema wakopeshaji binafsi hawajaguswa na sheria hiyo.

“Katika mabadiliko ambayo yameletwa na Waziri wa Fedha na Mipango (Dk Philip Mpango) jambo hili limeingizwa, watakuwa wanasimamiwa na sheria hii,”amesema.

Amesema pia katika mabadiliko yaliyoletwa na Serikali bungeni leo Ijumaa wakopeshaji wa mazao wameingizwa katika usimamizi wa sheria hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz