Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT: Serikali imewasahau wakulima wa pamba

Pamba Cotton.jpeg ACT: Serikali imewasahau wakulima wa pamba

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema kuwa serikali inapaswa kuchukua hatua kulinusuru zao la pamba ambalo bei yake inashuka kwa kasi kila mwaka.

Akizungumza na wananchi wa Kata Banemhi katika Jimbo la Bariadi, Ado amesema kuwa Serikali inapaswa kuongeza ruzuku au kuanzisha utaratibu wa fao la bei ili kupandisha bei ya zao la pamba.

Ado amesema kuwa amesikitishwa sana kuona zao la pamba ambalo awali lilijulikana kama dhahabu nyeupe likitelekezwa na Serikali.

"Nimejulishwa kuwa mwaka huu, Pamba inauzwa kwa Wastani wa Tsh. 1000. Hata viwanda vya kuchambua pamba vingi vimekufa na hakuna mkakati wa serikali wa kuvifufua. Kwa ujumla Serikali imemtelekeza Mkulima wa Pamba" Amesisitiza Ado.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live