Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kichapo cha Joshua chaibua utata

Joshua 09 26 At 12.jpeg Kichapo cha Joshua chaibua utata

Thu, 26 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya bondia Daniel Dubois kushtua dunia kwa kumchapa mwingereza mwenzake, Anthony Joshua usiku wa kuamkia Jumapili, mambo kibao yameibuka kuhusu  mapambano yajayo ya uzito wa juu duniani.

Inaelezwa promota wa Joshua, Frank Warren fasta sana ameitaka IBF iliyomkabidhi mkanda wake Dubois ihakikishe bondia huyo anapigana kwanza na Oleksandr Usyk anayejiandaa kupigana na Tyson Fury, mwezi Desemba.

Je IBF wataweza kuzuia pambano kati ya Usyk na Tyson kutofanyika ili mwenye mkanda Dubois apigane kwanza na Usyk?

Hilo linaonekana kuwa jambo gumu kutokea kutokana na kilichotokea awali walipomtaka Usyk achague kupigana na Dubois au auachie mkanda wa IBF, na bondia huyo wa Ukraine akafanya uamuzi mgumu wa kuuachia mkanda huo ili kufuata matakwa ya mkataba aliousaini wa kurudiana na Fury, Desemba, mwaka huu.

Upande wa pili, promota wa Joshua, Eddie Hearn naye amekuja na mpya kwa kusema kuwa hawakuweka kipengele cha pambano la marudiano (clause) kati ya Dubois na Joshua kiasi cha kuonekana kama ni majuto kwao wakitarajia Joshua angemshinda Dubois, lakini matokeo yakawa kinyume na matarajio na hata wapenzi wengi wa masumbwi ambao walimpa zaidi nafasi Joshua kushinda.

Hii inamaanisha nini? Hearn na upande wa Joshua sasa wanafanya mpango wa kuzungumza na promota wa upande wa Dubois, Frank Warren ili mabondia hao wazichape pambano la marudiano mwishoni mwa mwaka huu au hata ikitokea mapema mwakani wakati wakisubiri mbabe wa pambano kati ya Usyk na Tyson, Desemba, mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live