Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
BodyBuilding

Wenye mili mikubwa, watunisha misuli kukiwasha Desemba 3

Misuli Pic Data Kikao na wanahabari

Sun, 26 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Disemba 3, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kutakuwa na mashindano mbalimbali ya watu wenye mili mikubwa (Boardgard) na wale watunisha misuli ambalo litaandaliwa na (Strongest Man Challeng in Tanzania).

Meneja masoko wa Strongest Man Challenge in Tanzania, Fred Mwakisitu amesema shindano hilo linadhumini la kumtafuta mtu mwenye nguvu zaidi nchini awe mwanaume au mwanamke.

Mwakisitu amesema michazo ambayo itachezwa ni mtu mmoja kufunga kamba kwenye gari na kulivuta mwenyewe, kuamisha vitu vizito kutoka katika eneo moja kwenda lingine, kurusha tufe lenye uzito zaidi, kulala chini gari kupita juu yake pamoja na mengineyo.

Alisema ili kushiriki mchezo huo vigezo vyake vinatakiwa mshiriki awe na afya njema, watu wenye nguvu, mabaunsa, watunisha misuli, wanafunzi wa vyuo, wabeba mizigo mikubwa wale masokoni na mwananchi yoyote ambaye anajiamini anaweza kucheza.

"Katika shindano hili kutakuwa na hatua tatu tofauti tutaanza na ile ya awali ambayo uzito wa kitu kinachofanywa au kubebwa hakitakuwa mkubwa zaidi kama ule wa hatua ya tatu," amesema Mwakisitu na kuongeza;

"Yule ambaye ataweza kufanya mashindano yote hayo matatu kwa muda mchache ndio atakuwa mshindi wetu na atapata zawadi kubwa kulingana na kazi ambayo atakuwa ameifanya."

Mwenyekiti wa mabodigadi nchini, Faraji Robart alisema awali walikuwa hawana mashindano rasmi kutokana na miili yao ilivyo zaidi ya kufanya kazi ya ulinzi wa watu binafsi na maeneo mengine.

"Haya mashindano yanakwenda kutupa ajili nyingine kama vijana ambao wengi wao tupo mtaani na tunaomba Strongest Man Challeng in Tanzania wasiishie hapa waendelee mbele zaidi kwani tunaweza kupata wawakilishi wa nchi katika mashindano ya Olimpic," amesema Robart.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz