Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
BodyBuilding

Mtunisha misuli wa Marekani Afariki

Cedric McMillan Has Passed Away Cedrick McMillan

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtunisha misuli wa Marekani Cedrick McMillan amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kiafya yaliyosababishwa Uviko 19 pamoja na ajali ya barabarani.

Millan, ambaye ni mwanajeshi Mkongwe wa Marekani, alitwaa tuzo ya kutunisha misuli ya Arnold Classic mnamo mwaka 2017 ambayo iliandaliwa kwa heshima ya mcheza filamu na Gavana mstaafu Arnold Schwarzenegger.

Waandaaji wa Arnold Classic wameelezea kifo chake kama cha kusikitisha wakimuelezea Milan kama mtu mcheshi na mwenye bashasha.

Milan, aliyefariki juzi Aprili 12, 2022 akiwa na umri wa miaka 44 alishinda michezo mbalimbali ya kutunisha misuli na anakuwa mtunisha misuli wa tatu kufariki Nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Watunisha misuli wengine George Peterson na Shawn Rhoden pia walifariki kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live