Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
BodyBuilding

Aliyejidunga sindano kutunisha misuli afariki dunia

Valdir Segato 00 Aliyejidunga sindano kutunisha misuli afariki dunia

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtunisha misuli maarufu nchini Brazili, Valdir Segato amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 55 baada ya kutumia sindano kujidunga (Synthol injections) kwa miaka kadhaa ili kutunisha misuli yake.

Setago maarufu kama ‘Valdir Syntho’ alikuwa maarufu Zaidi katika mtandao wa TikTokn alianza kuugua na afya yake kutetereka kuanzia Julai 26, mwaka huu na kukimbizwa katika Hospitali ya UPA Nelson Mandela.

Inaelezwa kuwa, hapo awali, Valdir Segato alikuwa akienda gym kutengeneza misuli yake, lakini baadaye hakuridhishwa na namna misuli hiyo ilivyokuwa ikijijenga hivyo akaamua kuanza kutumia dawa ya kujidunga ili kuharakisha zoezi hilo na kuitengeneza misuli yake namna anavyotaka bila kujali madhara ambayo angeyapata baadaye.

Mwaka 2016, watalaam wa mazoezi walimshauri Setago kuachana na matumizi ya dawa hizo kwani yana madhara makubwa ikiwemo maambukizi, kuharibu mishipa ya damu na misuli iwapo ataendelea nazo lakini alipuuza akiamini kuwa dawa anazotumia zimethibitishwa na hazina madhara kwake huku akimtaja Arnold Schwarzenneger na Hulk toka filamu za Marvel's kuwa role model wake.

Setago Baada ya kuzidiwa na kukimbizwa hospitali, alibainika ana matatizo na kushindwa kupumua vizuri huku madaktari wakibainisha kuwa ni shambulio la moyo. Setago aliwahi kusema alikuwa anapenda watu kumsifia mwili wake na kumpa attention.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live