Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Zisikie ndoto za MVP Kikapu Mbeya

Mvp Zisikie ndoto za MVP Kikapu Mbeya

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuchaguliwa mchezaji bora wa ligi ya Kikapu Mkoa wa Mbeya (MVP), Gasper Benedict amesema haikuwa kazi rahisi kwake kutokana na upinzani aliokutana nao, huku akieleza ndoto zake kucheza mpira wa kulipwa nje ya nchi.

Nyota huyo alichaguliwa juzi wakati timu yake ya Crescent ikikabidhiwa kombe baada ya kufanya vizuri kwenye ligi hiyo wakimaliza vinara baada ya kulikosa taji hilo kwa miaka 10 mfululizo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Benedict alisema mafanikio hayo yamemuongezea ari, morali na matumaini katika kuendelea kufanya vizuri kwenye mchezo huo akieleza kuwa ndoto yake ni kucheza nje ya nchi.

Alisema baada ya mafanikio hayo pamoja na kuipa taji timu yake, kwa sasa anaenda kujipanga upya kuhakikisha anaendeleza kipaji chake kwenye michuano ya Taifa Cup itakayofanyika mkoani Mbeya mapema mwezi ujao.

“Haikuwa rahisi kwa sababu wachezaji wengi walionesha uwezo mkubwa na ushindani lakini nashukuru kwa nafasi hii ambayo inanipa nguvu zaidi kuendelea kupambania ndoto zangu,”

“Natamani siku moja kuona mpira wa kikapu Mbeya ukipiga hatua kubwa lakini nicheze nje ya nchi kuipeperusha bendera ya Tanzania, naenda kujipanga upya na Taifa Cup na nchi itanifahamu,” alitamba Staa huyo.

Katika hafla hiyo, Crescent ilikabidhiwa kombe lao kwa upande wa Wanaume baada ya kutwaa ubingwa, huku Tigers Queens nayo ikiweka ‘mwari’ wake kwa upande wa Wanawake.

Chanzo: Mwanaspoti