Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Warriors yabeba taji la NBA, Curry MVP

Championship Graphic 16x9 (600 X 337) Golden State Mabingwa NBA 2021/2022

Fri, 17 Jun 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mechi sita pekee zimetosha kwa timu ya Golden State Warriors kuwa mabingwa wapya wa ligi ya kikapu Marekani (NBA), kufuatia kuifunga timu ya Boston Celtics leo Ijumaa kwa pointi 103-90 kwenye mchezo wa sita wa fainali ya NBA.

Katika mchezo huo wa sita uliochezwa uwanja wa TD Garden ambao ni nyumbani kwa wapinzani wao Celtics, Warriors walifanikiwa kuongoza kuanzia robo ya kwanza hadi ya mwisho wa mchezo huo, ikiwa ni mwendelezo wa ubabe wa mechi tatu mfululizo.

Steph Curry, kwa mara nyingine tena ndiye ameibeba timu hiyo kwenye mchezo huo, kufuatia kuongoza kwa kufunga pointi 34 ambazo ni nyingi zaidi kwa mchezaji mmoja mmoja kwenye mchezo huo kwa timu yake, licha ya Jaylen Brown wa Celtics naye kufunga pointi hizo.

Warriors wanabeba taji la nne ndani ya miaka nane iliyopita, tangu mara ya mwisho walipobeba mwaka 2018, taji lao la tatu wakianzia 2015, 2017 na 2018 kabla ya kusubiri kwa miaka minne tena kubeba taji hilo lililokuwa mikononi mwa Milwaukee Bucks.

Celtics kwa upande wao, licha ya kupewa nafasi kubwa ya kufanya maajabu na pengine kubeba taji la 18 ambalo lingewapa rekodi ya muda wote kuwa timu ya kwanza kubeba mataji 18, wakibaki kulingana na Los Angeles Lakers kwa mataji 17.

Jayson Tatum, staa wa timu hiyo, kufunga pointi 13 pekee leo, kumechangia kwa kiasi kikubwa kupoteana kwa timu hiyo mbele ya Warriors ambao walitawala mchezo huo, wakifanikiwa kushinda katika uwanja wa ugenini, wakibeba taji mbele ya mashabiki wa Celtics waliokuwa na imani timu yao itashinda.

Wakati huohuo, staa Steph Curry amefanikiwa kutangazwa kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi wa fainali ya NBA, kufuatia ubora mkubwa aliouonyesha kwenye mechi tano kati ya sita za fainali hiyo iliyoishia mechi sita pekee.

Hiyo ni tuzo ya pili ya MVP kwa Curry kubeba ndani ya fainali mbili, ambapo awali alibeba tuzo hiyo ya MVP kwenye fainali ya ukanda wa Magharibi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz