Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Wachezaji Timu ya Mali wachapana konde kavukavu

Mali Mlok Wachezaji Timu ya Mali wachapana konde kavukavu

Fri, 30 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa kikapu ya Mali, Salimatou Kouroumana na Kamite Elisabeth Dabou waliingia kwenye mzozo na kupelekea kurushiana ngumi baada ya kupoteza kwenye mchezo wa Kombe la Dunia siku ya Jumatatu.

Mali ilipokea kichapo cha 81-68 dhidi ya Serbia ikiwa ni kipigo cha nne mfululizo kwenye michuano hiyo huko Sydney, Australia.

Mzozo huo ulizuka wakati kinara wa magoli wa mchezo huo Sasa Cado alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha michezo cha Serbia Sportklub, hotuba yake ilikatizwa na mzozo mkubwa kutoka kwa wachezaji wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live