Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Thompson amsifu Curry kwa kiwango bora

Curry.jpeg Steph Curry kushoto, Klay Thompson kulia

Sat, 11 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Golden State Warriors Klay Thompson amesema kwenye mchezo wa 5 wa fainali ya NBA wanapaswa kufunga zaidi ili kumsaidi Stephen Curry ambaye amekuwa akifunga alama nyingi kwenye kila mchezo.

"Steph ametubeba katika nyakati nyingi, mechi ya tano, itabidi tumsaidie. Kumwomba afunge alama 43 kila usiku ni kichekesho. Ni faraja sana kutazama kile anachofanya. Hufanya mara nyingi sana kiasi kwamba unachukulia kawaida.” Amesema Thompson

Curry amefunga alama 43 kwenye mchezo wa 4 wa fainali dhidi ya Boston Celtics alfajiri ya kumkia leo, mchezo ambao Golden State wameshinda kwa alama 107 kwa 97 na kufanya timu hizo kuwa zote zimeshinda 2-2 kwenye michezo 4 katika mfululizo wa michezo 7 ya fainali.

Kwenye mchezo huu Stephen Curry amefunga alama 3 (three-pointers) mara 7 katika majaribio 14 aliyofanya. Lakini pia kwenye mfululizo huu wa michezo ya fainali amefunga alama 3 mara 25 katika majaribio 51.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live